top of page

Amana ya Kontena Imekuwa Adha — VCS Ndiyo Dawa

  • Writer: VIASERVICE TANZANIA
    VIASERVICE TANZANIA
  • 3 days ago
  • 1 min read

Tatizo Halisi la Biashara:

Kila mfanyabiashara anayeshughulika na uingizaji wa bidhaa Afrika Mashariki anajua maumivu ya amana ya kontena. Kabla ya kupewa kontena, kampuni za meli zinahitaji uwekaji wa dhamana ya fedha — mara nyingi kati ya USD 1,000 hadi USD 3,000 kwa kila kontena. Kwa mfanyabiashara anayeshughulikia kontena 10 au 20 kwa wakati mmoja, hii inakuwa mzigo mkubwa wa mtaji uliozibwa/kufungwa.


Matokeo ni wazi:

  • Mtaji umezibwa/umefungwa badala ya kutumika kukuza biashara

  • Uwezo mdogo wa ushindani dhidi ya makampuni makubwa

  • Mtiririko mbaya wa fedha hasa kwa biashara za msimu

  • Fursa zinapotea kwa sababu mtaji haupatikani wakati unahitajika


VCS — Suluhisho la Kisasa:

Viaservice Kontena Solution (VCS) inakuja kutatua tatizo hili moja kwa moja. VCS ni suluhisho kamili la uendeshaji linalomuwezesha wakala wa forodha au msafirishaji kutoa na kuclear kontena bandarini — bila kuweka pesa taslimu kama deposit. Mtaji wako unabaki mkononi mwako, ukifanya kazi kwenye biashara yako, huku shughuli za forodha zikiendelea bila usumbufu wowote.


Kampuni kubwa za meli zinazoshiriki katika VCS:

Kenya: Blue Funnel (ESL), CMA-CGM, MSC, ONE, WECLINES

Tanzania: MSC, CMA-CGM, MAERSK, PIL, MESSINA, WOSAC (ONE Tanzania), Blue Funnel, WECLINES

Makubaliano zaidi yapo njiani kukamilika — ushirika unakua haraka.


Faida Zinazoonekana Mara Moja:

✅ Hakuna amana ya pesa taslimu

✅ Mtaji wako unabaki mkononi mwako

✅ Mwendo wa haraka wa forodha

✅ Uhusiano bora na kampuni za meli

Comments


bottom of page