top of page

Viaservice Kenya Yaingia Ushirika na Blue Funnel Kenya — Ukombozi Mpya kwa Wasimamizi wa Forodha Mombasa

  • Writer: VIASERVICE TANZANIA
    VIASERVICE TANZANIA
  • Jun 2
  • 1 min read


Habari Kuu:

Viaservice Kenya imefanya hatua kubwa katika sekta ya usafirishaji wa bahari Afrika Mashariki. Kampuni imeingia makubaliano rasmi na Blue Funnel Kenya — mawakala rasmi wa Emirates Shipping Line (ESL) Kenya — ili kuleta suluhisho bunifu linaloitwa Viaservice Kontena Solution (VCS) kwa wasimamizi wa forodha wanaofanya kazi bandarini Mombasa.


Makubaliano haya, yaliyoingiwa mwezi Aprili 2025, yanalenga kumfanya mteja wa forodha aweze kutoa au kuclear kontena za ESL bila kulazimika kuweka amana ya kontena (kontena deposit) — mzigo mkubwa wa kifedha ambao umekuwa ukizuia ukuaji wa biashara nyingi ndogo na za kati katika eneo hili.


VCS Ni Nini Hasa?

VCS ni suluhisho kamili la uendeshaji linalomuwezesha wakala wa forodha au msafirishaji kutoa au kuclear kontena bandarini — bila kulazimika kuweka pesa taslimu kama deposit au amana. Badala ya mtaji wako kufungwa bandarini, unabaki mkononi mwako ukifanya kazi kwenye biashara yako. Hii inamaanisha mtaji huru zaidi, mtiririko bora wa biashara, na ufanisi mkubwa katika shughuli zote za forodha.


Blue Funnel — Mshirika Mwenye Uzoefu

Ingawa makubaliano ya Kenya ni mapya, Blue Funnel na Viaservice wana historia nzuri ya ushirika Tanzania ambapo wameshirikiana kwa zaidi ya mwaka mmoja. Uhusiano huu wa muda mrefu unaonyesha nguvu ya ushirikiano na uaminifu wa pande zote mbili.

Kwa wasimamizi wa forodha Mombasa, hii ni fursa ya kujiunga na mpango ambao tayari umefanya vizuri Tanzania na sasa unakuja Kenya na nguvu zaidi.



📞 Wasiliana nasi leo: www.viaservice.ch/service

 
 
 

Comments


bottom of page